Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Mabaki ya ndege ya kijeshi ya kubeba mizigo iliyodunguliwa.
Waziri wa Ulinzi nchini Ukraine amesema kuwa mojawapo ya ndege zake za kijeshi za kubeba mizigo imedunguliwa na wapiganaji wanaounga mkono Urusi ilipokuwa ikitua katika uwanja wa ndege wa Luhansk mashariki mwa taifa hilo.
Ndege hiyo ya jeshi la angani la Ukraine ilikuwa ikiwabeba wanajeshi pamoja na vifaa.

Ripoti zinaarifu kuwa wafanyikazi wa ndege hiyo pamoja na wajeshi wote 49 wamefariki.

Idara ya maswala ya kigeni mjini Washington ,Marekani imesema kuwa ina hakika kwamba mizinga pamoja na silaha nyengine kali zinazomilikiwa na wanamgambo wanaotaka kujitenga nchini Ukraine zilitoka nchini Urusi.
 
Msemaji wa Idara hiyo amesema kuwa mizinga iliokuwa katika kambi moja ya silaha za kijeshi kusini magharibi mwa Urusi iliondolewa katika kambi hiyo.Waziri wa maswala ya kigeni nchini Uingereza William Hague amesema kuwa kuingia kwa vifaa hivyo nchini Ukraine hakuwezi kukubalika.
CHANZO NI BBC SWAHILI

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top