Stori: Musa Mateja
STAA Bongo Fleva, Hamisi Mwinjuma, ‘Mwana FA’, anasakwa na watu wasiojulikana ili wamuue, baada ya kutumiwa ujumbe wenye vitisho hivyo katika akaunti yake ya mtandao wa Facebook.
Akizungumza na paparazi wetu Juni 11 mwaka huu, Mwana FA alisema alishangazwa kukuta ujumbe huo ambao hata hivyo, hajui aliyemtumia ni nani. Katika kutaka kuwaonyesha mashabiki wake juu ya ugumu wa kazi yao hiyo, msanii huyo ‘aliupost’ ujumbe huo katika akaunti zake kwenye mitandao ya Facebook na Twitter.
“Dah, nimeshangazwa sana na ujumbe huu, mwanzo nilipouona sikuuchukulia maanani, maana nilijua ni watoto wadogo tu wanachezea vitu wasivyovijua, hivyo nikaona nami niuweke kwenye peji zangu ili ndugu na mashabiki zangu waweze kujua namna kazi yetu ilivyokua na mazingira magumu.
“Lakini simu yako inanifanya sasa niogope, hivyo inabidi nifanye jitihada za kuripoti jambo hili kwenye vyombo vya usalama ili iwe fundisho kwa wengine,” alisema FA.
Ujumbe huo ulikuwa ukisomeka; “Sikupendi mbwa ww, lazima nikuchome bisu la tumbo kwenye show zako na li…. Huna elimu ww bali una kisomo, mshenzi mkubwa tutakupata shoga ww, hata Fiesta tutakukamata.”
BONYEZA HAPA

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment