Mwanafunzi
(Jina tunalihifadhi)(8) wa darasa la kwanza katika shule ya msingi
Nyakabale wilayani hapa amelishwa kinyesi chake baada ya kukutwa
anajisaidia kwenye kisima akiwa na wenzake wakitoka shuleni.
Kamanda
wa polisi mkoani wa Geita Joseph Konyo amesema kuwa tukio hilo
limetokea tarehe 11 mwezi huu majira ya saa 4 asubuhi ambapo mwanafunzi
huyo akiwa na wenzake watatu wakitoka shule kufanya usafi ,walipofika
eneo hilo mwanafunzi mwenzao alienda kujisaidia karibu na kisima hicho
cha Marco Maico.
Akielezea
zaidi kuhusu tukio hilo kamanda Konyo amesema mara tu mwanafunzi huyo
alipomaliza kujisaidia, Marco alipita na kukuta kinyesi hicho.
Mmiliki wa kisima hicho Marcp Maico alimwamuru azoe kinyesi chake kwa mkono kinyesi hicho.
Hata hivyo alipoenda kukitupa Marco akamwambia akile hadi kiishe.
Kutokana
na hofu ya kutaka kupigwa mwanafunzi huyo alilazimika kula kinyesi
chake huku wenzake wakimsubiri na baada ya kumaliza alienda nyumbani na
wenzake.
Baada
ya kufika nyumbani mwanafunzi huyo alimwambia mama yake Agnes
Lujaja(26) juu ya kilichotokea na mama yake akaenda kwa balozi wa nyumba
kumi kutoa taarifa ambapo akampa barua ya kumpeleka zahanati ya
Nyakabale kwa matibabu.
Baadaye balozi huyo alitoa taarifa kwa Polisi na baada ya muda walifika kwenye eneo la tukio na kumtia mbaroni mtuhumiwa huyo.
Na Valence Robert-Malunde1 blog- Geita
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment