Mambo
hadharani! Uhusiano wa staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael
‘Lulu’ na mshiriki wa Shindano la Big Brother Africa 2013, Amir Nando
umewekwa kweupe.
Kabla
ya wawili hao kufunguka, kulikuwa na madai mazito kuwa Lulu na Nando
‘wanachepuka’ mara tu baada ya Nando kutolewa BBA kwa ukosefu wa
nidhamu.
Kuna habari kuwa Nando ndiye aliyevujisha ishu hiyo, jambo ambalo Lulu hakupendezwa nalo hivyo kumpiga chini.
Baada
ya kunyetishiwa ishu hiyo, gazeti hili lilimtafuta Nando ambaye
mwanzoni alifanya kama utani akidai Lulu ni mwanamke anayefaa kuolewa
(wife material) lakini alipoulizwa kwa msisitizo, alikana kuwa na
uhusiano na mrembo huyo.
“Lulu
ni mkali, niko tayari kumuoa lakini sijamwambia, akikubali freshi
nitamuoa. Kwa sasa ni mshikaji wangu tu na napenda kazi zake. Huwa ni
mtu ambaye napenda kufuatilia ishu zake,” alisema Nando.
Kwa upande wake Lulu alishtuka na kudai kuwa aulizwe huyohuyo Nando na si yeye kwani haoni sababu ya yeye kuulizwa.
Alifunguka: “Hebu muulizeni Nando kama ni Lulu mimi au mwingine? Yeye akishatoa jibu sina la kusema.”
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment