Kufuatia tangazo la kazi lililotolewa na Kamishna Mkuu wa Uhamiaji la
tarehe 14 na 17 Februari, 2014 kwenye magazeti ya Habari Leo, Mtanzania
na Daily news; kuhusu kujaza nafasi ya Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji,
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi anawatangazia waombaji
kuangalia katika tovuti www.moha.go.tz na www.immigration.go.tz ambapo
majina ya wanaoitwa kwenye Usaili yameorodheshwa. Usaili utafanyika
tarehe 13 Juni, 2014, katika uwanja wa Taifa. Wasailiwa wote wafike saa
moja na nusu asubuhi.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment