Mbunge
Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Samwel Nassari amefunga ndoa na
Anande Nko kwenye Kanisa la Pentekoste lililopo Kilinga, Arumeru jijini
Arusha ikifuatiwa na sherehe kubwa iliyofanyika katika Viwanja vya
Usa-River Academy jirani na Hoteli ya Ngurdoto.Sherehe hiyo
ilianza mishale ya saa 7:00 mchana siku ya leo ambapo watu wote
walialikwa wakiwemo ndugu, marafiki, jamaa na wananchi wote wa Arumeru
Mashariki ambao wamepiga ‘mpunga’ wa kutosha na vinywaji hadi kila mtu
akaondoka akisema ‘Nassari ameacha historia’.
Post a Comment
Post a Comment