Wanasayansi hao walisema kuwa kahawa ina nguvu ya kuangamiza bakteria inayosababisha kuoza kwa meno na hivyo basi huweza kupunguza hatari ya kuoza kwa meno. Kulingana na watafiti hao uwezo huo huenda ukatokana na nguvu ya kahawa ya kupambana na vioksidishaji.
Vikombe 2-3 kwa siku
Wanasayansi hao walitahadharisha kuwa unywaji wa kahawa kwa wingi pia huzidisha hatari ya kuoza kwa meno. Baada ya utafiti wao wanasayansi hao walipendekeza vikombe viwili au vitatu vya kahawa kwa siku.
Utafiti huo ulichapishwa katika jarida la wanasayansi la "Letters in Applied Microbiology".
BONYEZA HAPA
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment