Mkuu wa idara ya kupokea
malalamishi ya umma, Bi Thuli Madonsela hivi leo anatarajiwa kutoa
ripoti ya idara hiyo kuhusu uchunguzi wa iwapo Rais Jacob Zuma alihusika
katika ufisadi.
Boma la Nkandla la kibinafsi la Rais Zuma lina nyumba kadhaa, na limewekwa mitambo ya kisasa ya kiusalama ili kumlinda Rais.
Kulingana na mwandishi wa BBC wa Afrika Kusini, Omar Murtasa, Waziri wa Ujenzi wa Kazi za Umma nchini humo Nthula Tsinthesi, ilikuwa muhimu kukarabati boma hilo kwa kiasi hicho cha pesa kwa sababu boma hilo limewahi kuvamiwa mara tatu na wahalifu.
Ukarabati huo wa boma la Rais ambao sasa umenukia kuwa kashfa umewafanya wengi kuhoji iwapo bwawa la kuogelea la kisasa lililojengwa kwa kiasi kikubwa cha pesa ni sehemu ya usalama unaotajwa.
Na pia kumekuwepo na habari zinazodaiwa kuwa katika ripoti hiyo ambazo zinadai kuwa Rais Zuma mwenyewe alitoaamri pesa za umma kutumiwa, ambacho ni kinyume cha kanuni za kazi yake.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment