Baba mzazi wa mtoto John akiwa amekaa na mwanae mara tu baada ya hukumu kutolewa
MWANAMKE
Mwanahawa Nassoro(32) Mkazi wa Mtaa wa Airport jijini Mbeya amehukumiwa
kutumikia kifungo cha miaka mitatu jela baada ya kupatikana na hatia ya
kunyanyasa na kumtesa mtoto.
Mwanamke
huyo alipandishwa katika Mahakama ya Mwanzo ya Mbeya mjini juzi
kutokana na kosa lililokuwa likimkabili la kumtesa mtoto John Paul(03)
ambaye ni mtoto wa kaka yake.
Akisoma
mashitaka mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Mbeya mjini, Salome
Mwakyosi, mwendesha mashitaka wa Polisi Kopro Anthon alisema mtuhumiwa
alitenda kosa hilo Machi 12, Mwaka huu kwa nyakati tofauti kwa kumfungia
ndani na kumnyima chakula kinyume cha sheria namba 241 ya makosa ya
jinai sura ya 16 ya kanuni ya adhabu iliyofanyiwa marekebisho mwaka
2002.
Alisema
Mjumbe wa Serikali ya Mtaa wa Airport, Rehema Mohammed ndiye aliyebaini
na kutoa taarifa kwenye uongozi wa Mtaa ambapo mtuhumiwa alikamatwa na
hatimaye kufikishwa katika kituo cha Polisi kwa ajili ya hutua za
kisheria.
Upande
wa Mashitaka ulikuwa na mashahidi wane, ambapo wawili kati yao ndiyo
waliotoa ushahidi ambao ni pamoja na Mjumbe wa Serikali ya Mtaa na Mtoto
aliyefanyiwa ukatili huo ambaye alimtambua mahakamani Shangazi yake
Mwanahawa licha ya kuwepo watu wengi.
Mtoto
huyo alifika mahakamani kutoa ushahidi baada ya afya yake kuimarika
kutokana na kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya.
Hakimu
alipomuuliza mtoto kuhusu mtu aliyekuwa akimpiga alimuonesha Mwanahawa
mara tatu ambapo alizidi kumuonesha Shangaza yake huyo.
Kwa
upande wake mtuhumiwa wa kesi hiyo alipoulizwa kuhusiana na kosa hilo
alikiri ambapo Hakimu aliridhika na ushahidi uliotolewa na pande zote
mbili ikiwa ni pamoja na kukiri kwa mtuhumiwa.
Kutokana
na ushahidi huo Mahakama hiyo na ilimtia hatiani mshitakiwa kwa
kumuadhibu kutumikia kifungo cha miaka mitatu jela ili iwe fundisho kwa
watu wanaofanya vitendo vya kikatili dhidi ya watoto.
Mwisho.
Na Mbeya yetu
|
Post a Comment
Post a Comment