Baada
ya Dogo Janja kuuomba msamaha kupitia vyombo vya habari uongozi wa Tip
Top Connection na Madee aliyemtoa Arusha, Boss wa Tip Top Connection
Babu Tale ameiambia tovuti ya Times Fm kuwa anataka rapper huyo aseme
ukweli wa yote aliyoyasema awali baada ya kutoka Tip Top.
“Babu Tale ameweka wazi vipengele ambavyo anataka Dogo Janja aviweke sawa.
“Dogo anatakiwa aseme kama
kweli aliibiwa, kama kweli alidhurumiwa na kama kweli hajawahi kuishi
nyumbani kwa Madee. Anatakiwa aongee dhahiri asifiche, aongee tu
ukweli.” Babu Tale ameeleza.
Amegusia pia tukio ambalo
lilimsikitisha zaidi wakati Dogo Janja anafanya kazi akiwa chini ya
menejimenti ya Mtanashati Entertainment.
“Siku zote kwenye ukweli
uongo hujitenga, wakati yuko South Africa alipost picha ‘ningekuwa Tip
Top nisingefika huku’. Nilishangaa heeh huyu kutoka huko kijijini kwao
alifanyaje hadi kufika hapa
“Wazazi wake nao wakawa
wamekubali uongo wa mtoto wao wakaanza kutuongelea na sisi maneno ambayo
ni uongo. Ulikuwa uongo wa watoto halafu bado wao wanakandamiza uongo
zaidi ya uongo. Kwa kuwa ni mtoto kuna wazazi ambao walisimama nyuma
yake ambao nao walikuwa wanasapoti. Aongee ukweli mimi ntamsaidia.” Babu
Tale ameeleza.
Babu Tale ameeleza kuwa Dogo
Janja ameshamtafuta kwa njia ya simu lakini amemwambia ujumbe ule ule
kuwa awaambie ukweli watanzania.
Kwa upande wa dogo janja,
ameongea na Tovuti ya Times Fm na hakutaka kuizungumzia kwa undani kauli
ya Babu Tale, zaidi alieleza kuwa alichokifanya kuomba msamaha
alimaanisha kuwa alikuwa amekosea na hakuna aliyemsukuma kufanya hivyo.
Ameeleza kuwa endapo
atakaribishwa tena Tip Top Connection atajiunga na kundi hilo japo
ameeleza kuwa kuomba kwake msamaha hakuwa na maana kuwa alikuwa na lengo
la kurudi Tip Top.
“Mimi nimeomba msamaha kwa
kuwa nataka kuweka mambo sawa na kumaliza tofauti na uongozi wangu wa
zamani. Hivyo tu. Wakinikaribisha Tip Top itakuwa poa tu pia…fresh.”
Times Fm ilimtafuta Madee
ambaye alisema kuwa bado hajawa tayari kuongelea suala hilo na kwamba
mtu anaeweza kuzungumzia suala hilo kwa sasa ni Babu Tale.
>>>>>Chanzo:TimesFm
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment