Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dr Seif Rashid amesema ugonjwa wa kifua kikuu ni ugonjwa wa tatu unaosababisha vifo vingi nchini Tanzania nyuma ya malaria na ukimwi,Dr Rashid aliyasema hayo wakati akitoa tamko kuhusu ugonjwa huo kwenye ukumbi wa wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii mjini Dodoma.

Kwa mujibu wa wizara hiyo takwimu zinaonyesha kuwa idadi ya wagonjwa wa ugonjwa wa kifua kikuu imeongezeka kutoka idadi ya 11,000 ya mwaka 1980 hadi idadi ya wagonjwa 63,892 mwaka 2012.

Akitaja sababu za kuongezeka kwa idadi hiyo,waziri huyo alisema ni pamoja makazi duni ya watu,msongamano wa watu hasa sehemu nyingi za mjini na wagonjwa wa ugonjwa huo kuchekewa kupatiwa matibabu kwa wakati sahihi.

Aidha Dr Rashidi ameitaja mikoa inayoongoza kuwa na idadi kubwa ya wagonjwa wapya kuwa ni Dar es salaam 13,983,Mwanza 5,946 na mkoa wa Shinyanga 4,074.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top