Mwanafunzi
wa Chuo Kikuu Dodoma – UDOM aitwae KAMUGISHA ISACK (24) Mhaya, Mwaka wa
Tatu Kitivo cha Sayansi ya Jamii (Social Science) anayeishi Block Namba
11, chumba Namba 62, alijitupa kutoka ghorofa ya pili hadi chini na
kusababisha majeraha sehemu za mdomoni, shingoni na kwenye paji la uso.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna msaidizi mwandamizi wa Polisi DAVID
MISIME amesema hili tukio limetokea terehe 18/03/2014 saa mbili na robo
chuo kikuu cha Dodoma kwa mujibu wa Sylvester Onesmo wa jeshi la Polisi Dodoma.
Amesema
uchunguzi wa awali umeonyesha chanzo cha tukio ni ulevi ambapo majeruhi
alilazwa katika hospitali ya UDOM na baadaye kuhamishiwa Hospitali ya
Mkoa wa Dodoma na kuruhusiwa tarehe 20/03/2014 baada ya kuonekana hali
yake inaendelea kuimarika.
Pamoja
na hayo, Kamanda MISIME amesema mtuhumiwa atafikishwa mahakamani baada
ya kukamilisha taratibu zote kujibu shitaka la kujaribu kujiua.
Post a Comment
Post a Comment