Waziri mkuu wa Australia amesema
kuwa mitambo ya satelite ya nchi hiyo imenasa picha za vitu
vinavyoonekana kama vifusi ambavyo huenda ni vya ndege ya Malaysia
iliyopotea siku 13 zilizopita.
Msemaji wa halmashauri ya usalama wa safari za ndege, John Young, baadaye alisema kuwa vifaa hivyo ambavyo kimoja kina ukubwa wa mita 24, vimeonekana umbali wa kilomita 2500 kusini Magharibi mwa pwani ya Australia.
Aliongeza kwamba,vifusi itakuwa vigumu kuviona vifusi hivyo na pia huenda sio vya ndege hiyo.
Wakati taarifa hii ilipotolewa, kulikuwa na ndege ya Australia katika neo hilo , ndege zaidi zinatarajiwa kuwasili katika eneo lenyewe na pia manowari ya jeshi inaelekea huko.
>>>bbcswahili
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment