Msanii wa filamu nchini Tanzania, Elizabeth Michael ‘Lulu’ ameonesha kuwaumiza vichwa watu baada ya kutweet kitu ambazo kilileta sintofahamu katika jamii inayomzunguka.
Akitolea ufafanuzi wa tweet aliyoiweka ambayo watu wamedai kuwa ni dongo amesema kuwa aliandika tweet hiyo kama utani na kusema kuwa huweza pia ikawa na ukweli ndani yake.
Amesema kuwa utani wake umefanya watu wamfikirie vibaya kuhusiana na viti maalum bungeni na kusema kuwa watu wengi wamekuwa na dhana tofauti kuwa viti maalum ni vya kupeana.
Amefafanua na kusema kuwa watu wamuelewe kuwa hajamsema mtu na kudai kuwa watu wasichukulie poa kama kila anayewekwa bungeni ni kutokana na sura nzuri au umbo zuri.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment