Home
»
SIASA
» Mpasuko CCM: Nchimbi, Sophia Simba na Adam Kimbisa Wapinga Jina la Edwarad Lowassa Kukatwa
Habari za Hivi punde kutoka makao makuu ya CCM mkoani Dodoma ni kwamba wajumbe wa kamati kuu watatu ambao ni Dkt. Emmanuel Nchimbi, Sophia Simba na Adam Kimbisa wamepinga maamuzi ya kamati ya kumkata mmoja wa wagombea maarufu na kumweka mgombea asiyekuwa maarufu.
Akizungumza usiku huu majira ya saa saba za usiku Dkt. Nchimbi amesema kwamba wao watatu hawajakubaliana na maamuzi ya kamati kuu iliyoketi usiku huu chini ya Mwenyekiti Dkt Jakaya Kikwete kumkata mgombea maarufu kwa manufaa ya mgombea asiye maarufu.
“Katika kikao cha leo kamati haikupoea majina yote yaliyojadiliwa na maadili, suala ambalo ni kinyume na kanuni, pili katiba ya CCM inataka mtu anayekubalika ndiye apewe nafasi ya kwanza, lakini kikao cha leo kimeonyesha kuminya wanaokubalika kwa manufaa ya wachache wasiokubalika” Amesema Dkt. Nchimbi.
Hivyo basi kwa sababu hiyo wao watatu ambao ni wajumbe wa kamati kuu wamewataarifu wenzao kwamba wamejitenga na maamuzi ya kikao hicho na kutangaza kuto kuyaunga mkono.
Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali za kisiasa nchini Tanzania zinaonesha kuwa mgombea anayekubalisa sana CCM ni Mbunge wa Monduli Edward Lowassa akifuatiwa na Waziri wa Mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Bernad Membe
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Je Umezisoma Hizi?
- Profesa Lipumba Asema Hana mpango wa kuhama CUF wala kuanzisha chama Kingine ........Ataja Sababu Zilizomfanya Amkatae Lowassa08 Sep 20160
Aliyekuwa mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba amesema hana mpango wa kuhamia chama choch...Read more ?
- Msajili amlima Barua Maalim Seif kuhusu sakata la Lipumba01 Sep 20160
Ofisi ya Msajili wa Vyama vya siasa nchini imemuandikia barua Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananch...Read more ?
- Breaking News: Mbowe Atangaza Kuahirisha Maandamano ya Oparesheni UKUTA Yaliyokuwa Yamepangwa Kufanyika Kesho31 Aug 20160
Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo ametangaza kusitishwa kwa maandamano ya Opare...Read more ?
- Hotuba ya Edward Lowassa alipokuwa Iringa Jana25 Aug 20160
Leo(Jana) nimewatembelea ndugu zangu wa Kilolo - Iringa kuwashukuru na kuwaeleza kuwa tu...Read more ?
- Prof Lipumba:Sihusiki na Vurugu zilizotokea Katika Mkutano wa CUF23 Aug 20160
Aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF Prof.Ibrahim Lipumba amesema hausiki na fujo wala vurugu zilizotokea ...Read more ?
- Mbunge kizimbani kwa maneno ya uchochezi23 Aug 20160
MBUNGE wa Jimbo la Tanga kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Mussa Mbarouk amefikishwa katika Maha...Read more ?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment
Post a Comment