March 21, 2025 10:37:53 PM Menu
 

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Staa mkubwa wa Bongo Movies, Jacob Stephen ‘JB’ amekanausha taarifa za kutaka kugombea ubunge jimbo la kinondoni ambazo zimekuwa zikienea kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii.

JB ameeleza kuwa japo watu mbali mbali wamekuwa wakimfuata na kumtaka agombee yeye amekuwa akiwashukuru na kuwaeleza kuwa anaipenda sana kazi yake ya uigizaji.

Kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa Instagram aliyaeleza hayo akiwa anatolea ufafanuzi kile ‘mrekebishatabia’ alichokiandika kwenye mtandao huo.

@mrekebishatabia,  Na mimi nimezisikia habari hizo eti nataka kugombea k,ndoni. si za kweli ingawa kuna kundi kubwa lilinifata na kunishawishi nigombee lakini niliwajibu nashukuru kwa kunifikiria lakini nafurahia kazi ya uigizaji kuliko kazi nyingine...

Awali ‘mrekebishatabia’ alitoa orodha ya wasanii wanasemekana kuwania ubunge ambapo aliandika;

Kwa mujibu wa jamiiforums hawa ndo wasanii wanaowania kugombea Ubunge 2015
1. Prof Jay- Mikumi
2. Dude- Tabora Mjini
3. JB- Kinondoni
4. Soggy doggy- Segerea
5. Steve Nyerere - Kinondoni
6. Afande Sele- Morogoro Mjini
7. Dokii- Kilosa Morogoro
8. King majuto- Tanga Mjini
9. Shilole- Igunga
10. Kalapina- Kinondoni
11. Baba Levo (haijawekwa wazi)
12. Juma chikoka-Ilala
13. Kingwendu- hajaweka wazi jimbo
14. Wema sepetu- Singida
Mwingine nani??? Mambo yanaelekea yatachanganya hapo baadae. Kila la heri wasanii wote.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro
21 Jun 2015

Post a Comment

 
Top