Mbunge wa Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi (Sugu) ameshinda kesi aliyomfungulia aliyewahi kuwa mchumba wake Faiza Ally ambaye pia ni mama wa mtoto wake wa kike aitwaye Sasha.
"Sijapewa nafasi nimepelekwa mahakamani ijumaa na leo jumanne nimepewa hukumu/ mwanangu achukuliweβ¦.. hapana ! sitarudi nyuma na haitakua rahisi ninakata rufaa na kutafuta wakili wa kunisimamia hili.
"Mwanangu anasoma vizuri anaishi vizuri na naamini kwenye mikono yangu yuko salama zaidi ya kokote/ yaani kuhusu kukosa kukaa na mwanangu ni bora kufa kuliko kuishi nikimuona sasha ana lelewa na mama mwingine ikiwa mimi mama yake niko hai na makini katika malezi ya mtoto wangu.
"Nina ndoto na mwanangu nyingi sana , nahitaji kuishi nae yeye ndio kila kitu kwenye maisha yangu/ nampenda sana mwanangu na sijashindwa kumlea.
"Naona uchungu sana kupelekwa mahakamani na kupokonywa mtoto wangu bila sababu za msingi .
"Sitaogopa cheo chake cha ubunge kamwe ntasimama kama mama mwenye haki kwa mtoto wake β¦mungu naomba nielekeze.nisimamie na unihukumie huu ukatili ninao fanyiwa na baba sasha β¦..β
Post a Comment
Post a Comment