March 16, 2025 04:18:40 PM Menu
 

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Mkuu wa Kitengo cha habari na Mawasiliano wa Klabu ya Yanga,Jerry Muro amekanusha kutimuliwa kwenye klabu hiyo kwa utovu wa nidhamu.

Taarifa zilizoandikwa na gazeti la Uhuru zinasema kuwa habari kutoka kwa mmoja wa viongozi wa klabu hiyo,ambaye hakutaka kutajwa jina lake kwa kuwa si msemaji alisema kuwa Muro ametimuliwa baada ya kufanya kazi kinyume na maagizo ya uongozi wa klabu hiyo.

Kiongozi huyo alisema kikao cha dharura cha kumfuta kazi kilifanya juzi jioni kabla ya maazimio kupelekwa kwa mwenyekiti wa klabu hiyo.Yusuf Manji.

Baada ya taarifa hizo Jerry Muro alijibu tuhuma kwa kusema hivi… Ndugu zangu nimepigiwa Simu nyingi Sana na asubuhi hii nimeona Kwenye gazeti ka uhuru kuhusiana na taarifa zangu za kuondoka Yanga wakati natafakari hatua za kuchukua dhidi Ya upotoshaji huu wa Habari naomba niseme Jambo moja Muhimu mimi Bado Niko Yanga Kama Mkuu wa idara Ya Habari na Mawasiliano na mimi Bado mwanachama hai wa Yanga Mwenye kadi No 028508 Niko Yanga na nitaendelea kuwa Yanga Miaka mia,wasalamu jerry muro….

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro
18 Jun 2015

Post a Comment

 
Top