Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Baadhi ya wanafunzi waliouawa au kujeruhiwa darasani

**********  
Katika style kama ile ya shambulizi la Westgate Mall, wanamgambo wa al-Shabaab wamevamia na kushambulia  chuo  kikuu  cha  Garissa kilichopo katika mji wa Garissa. Zaidi  ya watu 15 wameuawa, na wengine zaidi ya 53 wamejeruhiwa.

Mkuu wa jeshi la polisi Kenya, Inspector General Joseph Boinnet amesema kuwa magaidi hao walivamia geti kuu la chuo hicho na kuwarushia risasi walinzi alfajiri saa 5.30, wakati wanafunzi wa Kiislam wakienda kwenye swala ya asubuhi.
Polisi waliokuwepo chuoni hapo walikimbilia katika eneo la tukio na kuanza kurushiana risasi na magaidi hao, ambao walifanikiwa kuingia kwenye mabweni ya wanafunzi.

Polisi wa ziada na wanajeshi waliitwa kuja kusaidia na mirindimo ya risasi ilisikika kati ya wavamizi hao, polisi na wanajeshi.
Wanafunzi waliokuwa wakipiga simu kutoka ndani ya mabweni wamesema kuwa kuna majeruhi wengi sana. 
Wanafunzi waliofanikiwa kutoroka wamesema kuwa idadi ya wavamizi hao ni angalau watano  na bado kuna wanafunzi na maprofesa wengi wanashikiliwa mateka.

Taarifa za hivi punde zinaarifu kuwa magaidi hao wameanza kuwachinja baadhi ya mateka waliowashikilia.
Mateka mmoja (mwanafunzi) mwenye asili ya Somalia aliyeachiwa huru na magaidi hao ameviambia vyombo vya habari vya Kenya kuwa wanafunzi kadhaa wamekwishauawa na miili yao imetapakaa ndani ya vyumba na madarasa huku zoezi la Uchinjaji wa mateka wengine walio hai likianza.


Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ametuma salamu za rambi rambi kwa familia za wale waliouawa katika shambulizi hilo.

Kenyatta amewataka wakenya kuwa watulivu wakati huu ambapo maafisa wa usalama wanakabiliana na wapiganaji hao. 

Wanajeshi wa jeshi la Kenya katika geti la chuo hicho



Baadhi ya miili ya marehemu waliouawa katika shambulio la al-Shabaab katika chuo kikuu cha Garissa




Helicopter ya jeshi ikitua na maiti na baadhi ya majeruhi katika kambi ya jeshi la Langata




Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Excel, iliopo karibu na chuo kikuu cha Garissa wakiondolewa kutoka shuleni kuhakikisha usalama waoAn injured woman is wheeled to a plane to be airlifted to Nairobi for treatment following the
Majeruhi akipatiwa matibabu

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top