Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Takriban watu 15 wanaodaiwa kufunika nyuso zao wameshambulia chuo kikuu cha Garrissa Kaskazini mashariki mwa Kenya.
Watu hao wanadaiwa kuingia katika taasisi hiyo mwendo wa saa kumi asubuhi wakati ambapo waislamu walikuwa wakifanya sala yao ya alfajiri.

Kufuatia shambulizi la chuo kikuu cha Garissa ,Shirika la msalaba mwekundu Red Cross limewataka raia wa Garissa kutoa msaada wa damu.
Walioitikia wito huo tayari wameeleka katika hospitali kuu ya Garissa mbapo kituo cha kutoa damu kimeanzishwa chini ya mti.

Mwanafunzi wa chuo kikuu cha Garissa Collins Wetangula amesema kuwa wakati wapiganaji hao walipoingia katika nyumba anayolala aliwasikia wakifungua milango na kuwauliza watu iwapo ni waislamu ama wakristo.
''Kama wewe ni mkristo unapigwa risasi papo hapo.Kila mlio wa risasi nilipousikia nilidhani nitauawa'',ameliambia shirika la habari la AP.
Amesema kwamba maafisa wa usalama baadaye waliingia kupitia dirisha moja na kumtoa yeye na wenzake hadi katika eneo salama.

Mwandishi wa habari wa Kenya Dennis Okari ambaye yuko katika eneo la chuo kikuu cha Garissa ameandika katika mtandao wake wa Twitter akisema kuwa:
Wapiganaji hao wako katika jumba la kulala wanafunzi .''Ninaweza kusikia milio ya risasi kutoka upande wa pili.@ntvkenya".

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top