Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Katibu mkuu wa CHADEMA, Dr Slaa, ametoa madai mapya ya kuongezewa mshahara na stahiki zake kufuatia mafanikio aliyoyapata ya kuongezewa mshahara katika madai yake yaliyopita ambayo yalikuwa ni ongezeko la asilimia 40 tu ya kile kiwango alichokitaka!

Mchanganuo sahihi wa mshahara wa katibu mkuu wa CHADEMA na stahiki zake:

Mshahara anaolipwa Dr Slaa kwa sasa ni Tshs. 9,300,000 kwa mwezi wakati kabla ya madai yake ya mara ya mwisho alikuwa akilipwa Tshs. 6,600,000. Ambalo ni ongezeko la 40%.

Stahiki za Dr Slaa kama Katibu Mkuu:

Dr Slaa anawekewa kiasi cha lita 1000 za mafuta ya Petrol kila mwezi ambayo kwa wastani ni Tshs milioni 2,000,000 katika gari lake alilokabidhiwa na chama ambalo pia ulitumia kwa shughuli zake binafsi na za chama. Ifahamike, hii ni nje ya mshahara!

Haijaishia hapo, Dr Slaa pia anapewa pesa kiasi cha Tshs 2,500,000 kama fedha ya matumizi ya ofisi ya katibu mkuu wa chama kila mwezi. Hii pia ipo nje ya mshahara wake na matumizi yake hayaeleweki.

Kama hiyo haitoshi, Dr Slaa kila afanyapo vikao vya chama vya ngazi mbalimbali uinuka na wastani wa Tshs. 1,500,000 kwa kikao kimoja.

Madai Mapya:

Mshahara: Dr Slaa kwa sasa ameitaarifu CHADEMA kuwa wakati wa kukamilisha asilimia 60 zilizobaki za madai yake ya awali ya mshahara wake umewadia. "Hii ni kutokana na ongezeko la gharama za maisha na pia kuongezwa mkataba wa kutumikia chama kwa nafasi ya ukatibu mkuu" alieleza Dr Slaa.

Hivyo basi, kama CHADEMA itaridhia madai hayo mapya na kumuongeza Dr Slaa kiasi cha asilimia 60 kilichobaki, Dr Slaa ndiye atakuwa katibu mkuu wa chama cha siasa anayelipwa pesa nyingi kuliko wote katika nchi za ukanda wa Afrika mashariki! Kiasi hicho kitafikia Tshs. 13,200,000 kwa mwezi huku kikienda sambamba na kuongezeka kwa posho na stahiki zingine.
By PATIENT ZERO-JF

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top