Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Kilichojificha nyuma ya pazia la uhusiano wa mastaa wa Bongo, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’, na Shamsa Ford sasa kimevuja baada ya mtandao huu kunasa habari za wawili hao kuwa kwenye uhusiano wa mapenzi kiasi cha kudaiwa kupika na kupakua pamoja.



Chanzo  kimeeleza kwamba, wawili hao ambao kila mmoja katika siku za hivi karibuni aligombana na mwenza wake wa awali, wamekuwa katika uhusiano wa kimapenzi kwa uficho wa hali ya juu, wakionekana mara kwa mara nyumbani kwa Mbongo Fleva anayeishi Kimara Korogwe, jijini Dar.
Inadaiwa kuwa kwa zaidi ya wiki tatu sasa wawili hao wamekuwa wakionekana katika gari moja, wakitoka au kuingia nyumbani kwa Nay wakitokea mjini kwenye mihangaiko yao ya kila siku.
“Kama ulikuwa hujui vizuri naomba nikujuze, Nay na Shamsa wanaonekana walikuwa wakifuatiliana kwa muda mrefu, nasema hivi kwa vile siku chache tu baada ya wawili hawa kuachana na watu wao wa zamani, leo wako pamoja tena wanaonyeshana mahaba utadhani walikuwa pamoja miaka mia iliyopita,” alisema mtoa habari wetu.

Ili kuthibitisha maneno yake, chanzo chetu kilituma picha kadhaa za wawili hao wakiwa nyumbani kwa Nay, huku akisisitiza kuwa hata dada na ndugu wa mwanaume huyo, nao wamekuwa wakipost picha za Shamsa ambaye hivi sasa anapika na kupakua nyumbani kwa mkali huyo wa kibao cha Nakula Ujana.
Nay wa Mitego alipoulizwa kuhusu ukaribu huo, alisema hadhani kama ni jambo la haki kwake kuulizwa kuhusu suala hilo, wakati inajulikana kuwa yupo ‘single’.
“ Bwana eeh mimi na Shamsa ni wasanii halafu ukiachia mbali hilo kuwa karibu naye si tatizo wala sioni cha ajabu maana yeye yupo single na mimi nipo single labda kama kuna kipya hapo unaweza kuniambia nikakuelewa, ila ishu ya kuja kwangu au mimi kuwa kwake sioni kama ni ishu,” alisema.



Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top