Wachezaji wa Simba SC wakimpongeza Okwi leo Jumamosi March 14, 2015, baada ya kufunga bao pekee la ushindi dakika za lala salama dhidi ya Mtibwa Sugar…ambapo BAO la Emmanuel Anord Okwi dakika ya 90 ushei limeipaSimba SC ushindi wa 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jioni hii katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Simba SC sasa inafikisha pointi 29 baada ya mechi 18 na kuendelea kukamata nafasi ya tatu, nyuma ya mabingwa watetezi, Azam FC pointi 30 za mechi 16 sawa na vinara Yanga SC, wenye pointi 31.
Okwi alifunga bao hilo, wakati tayari baadhi ya wapenzi wa Simba SC wameanza kutoka uwanjani, wakiamni matokeo ni sare.
Mganda huyo, alifunga baada ya kupata pasi ya Abdi Banda na kumchambua vizuri kipa aliyefanya kazi nzuri leo, Said Mohamed Kasarama.
|
Post a Comment
Post a Comment