March 26, 2025 06:09:20 AM Menu
 

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Charles Mihayo, (36) mzaliwa wa Tanzania ambaye mwezi April, 20, 2014 aliwauwa watoto wake wawili wadogo wa kike nyumbani kwake huko Melbourne, Australia (Ingia hapa) amehukumiwa kifungo cha maisha.

Inadaiwa kuwa baada ya kuachwa na mke wake, hasira zilimfanya bwana Mihayo kuamua kufanya ukatili wa kukatisha uhai wa watoto wake mwenyewe Savannah (4) na Indianna (3), ili tu kumuumiza mke wake kama njia ya kumlipizia kisasi. Inadaiwa kuwa aliwauwa kwa kuwakandamiza na mto baada ya kucheza nao.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa siku mauaji hayo yalipofanyika, mama wa watoto hao aliwapeleka kwa baba yao bwana Mihayo. Baada ya kuwafikisha baba yao aliwafanyia shopping ya nguo na viatu vipya.

Kabla ya kutenda ukatili huo kwa damu yake mwenyewe, Mihayo aliwarekodi video wakicheza muziki huku akicheza nao. Na katika video ambayo polisi baadae waliiona, alisikika akiwaambia binti zake wamuoneshe mama yao nguo mpya alizowanunulia, na walifanya hivyo na kisha mwanaume huyo akakaa mbele ya camera na kusema “tutamuonesha mama kitu kingine dakika kumi zijazo”, na kuendelea kucheza nao hadi alipowakandamiza na mto (pillow) hadi kufa.

Baada ya kufanya mauaji Mihayo mwenyewe aliwapigia simu polisi ambao baada ya kufika nyumbani kwake wakiwa mlangoni aliwaambia , “Tayari, nimewaua. Nimewaua watoto wangu. Inabidi mumuulize huyu [mama yao] sababu.”

Polisi waliwakuta watoto hao wakiwa tayari wamefariki huku wakiwa wamevalishwa nguo na viatu vipya ambavyo walinunuliwa na baba yao siku hiyo.

Licha ya kuhukumiwa kifungu cha maisha, Charles Mihayo anatakiwa kutumikia kifungo cha miaka 31 kabla ya kupata haki ya kupewa msamaha.
UNGANA NASI KATIKA FACEBOOK

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro
20 Dec 2014

Post a Comment

 
Top