Arsenal imefanikiwa leo hii March 14, 2015 kupata ushindi mzuri dhidi ya West Ham ikiwa ni mchezo wa ligi kuu uingereza msimu huu wa 2014/2015 wakati pia ikijiandaa kwa mchuano wa kata na shoka kati yake na klabu ya Monaco siku ya jumanne March 17,2015 kwenye mashindano ya Klabu Bingwa Ulaya.
Kilabu hiyo ya Wenger iliishinda West Ham kwa mabao 3-0 na hivyobasi kujimarisha katika nafasi ya nne bora katika msimamo wa ligi ya Uingereza.
The Gunner ilitawala mechi hiyo huku Olivier Giroud akifunga bao la kwanza kabla ya kipindi cha kwanza kukamilika.
|
Post a Comment
Post a Comment