Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Wekundu wa Msimbazi Simba SC leo March 22, 2015,jioni , imezinduka kutoka kwenye kipigo cha 2-0 cha Mgambo Shooting wiki iliyopita, baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Ruvu Shooting katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara  msimu huu 2014/2015  kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Simba SC  ilipata bao lake la kwanza dakika ya 60, mfungaji Ibrahim Hajibu kwa mkwaju wa penalti, baada ya beki wa Ruvu, Said Madega kumfanyia madhambi Awadh Juma.

Dakika moja baadaye ya 61, Awadh Juma aliifungia Simba SC bao la pili baada ya kujipasia mwenyewe na kupiga shuti.

Mshambuliaji Elias Maguri aliyetokea benchi kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Mganda, Emmanuel Okwi aliipatia Simba SC bao la tatu dakika ya 75, akimalizia pasi nzuri ya Said Ndemla.

Kwa ushindi huo, Simba SC inafikisha pointi 32 baada ya kucheza mechi 20, ikiwa nyuma ya Azam FC pointi 36 za mechi 18 na Yanga SC pointi 37 za mechi 18 pia.

Kwenye mchezo mwingine wa Leo, Nao Mabingwa wtetezi ,Azam FC imeibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji Coastal Union, Uwanja wa Mkwakwani, Tanga katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara. 

Shukrani kwake, mfungaji wa bao hilo Nahodha John Raphael Bocco ‘Adebayor’ dakika ya 31 akimalizia pasi nzuri ya kiungo Mudathir Yahya.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro
22 Mar 2015

Post a Comment

 
Top