Kupitia akaunti yake ya Facebook, aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema) na Mwenyekiti wa Kamati ya PAC ambaye jana March 21,2015, alijiunga rasmi na Chama cha ACT-Tanzania, Zitto Kabwe amempongeza Amina kwa imani aliyopewa na wajumbe wenzake wa Pac.
"Nimefanya kazi na Amina tangu mwaka 2010 tulipokuwa kamati ya POAC na nina imani, kwa ushirikiano mkubwa wa Makamu Mwenyekiti ndugu Deo Filikunjombe wataendeleza kazi tuliyoianza ya kujenga mfumo madhubuti wa Uwajibikaji nchini kwetu" aliandika Zitto Kabwe.
|
Post a Comment
Post a Comment