March 15, 2025 03:43:47 PM Menu
 

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
bobbi-kristina

Bado kuna utata kuhusu kinaachoendelea juu ya afya ya Bobbi Kristina, mtoto wa pekee wa Marehemu Whitney Houston, mengi yanaendelea kuzungumzwa kuhusu hali yake huku wengine wakisema kuwa leo ni siku ambayo familia hiyo imeruhusu madaktari kumtoa mashine ya kupumulia ambayo aliwekewa toka siku ambayo alifikishwa hospitali baada ya kukutwa akiwa ameanguka ndani ya bafu, Georgia Marekani.
Baada ya yote kusikika familia ya Bobbi imeamua kutumia kampuni ya wanasheria wao kutoa maelezo rasmi kuhusu kila ambacho kimesikika juu ya hali ya mtoto huyo, taarifa hiyo imekanusha uvumi wote uliowahi kusikika ikiwemo ishu ya kumtoa mipira ya kupumulia siku ya leo ambapo ni siku ambayo mama yake alifariki.
Katika taarifa hiyo ya Wanasheria wa familia hiyo wamesema wanaangalia namna ya kuwachukulia hatu wote waliotoa taarifa za uongo ikiwemo waliosema walizungumza na wahusika wa familia hiyo kitu ambacho sio kweli.
whitney-bobbi-kristina
Marehemu Whitney Houston akiwa na mtoto wake Bobbi Kristine wakati akiwa mdogo.
TMZThe National EnquirerThe Atlanta Journal Constitution na the Daily Mailni sehemu ya vyombo vya habari ambavyo vimelaumiwa kwa kuandika taarifa za uongo.
ap_bobbi_kristina_oprah_jt_120311_wg
Bobbi Kristina akiwa na Oprah Winfrey

Bado hakuna taarifa rasmi ambayo familia hiyo imetoa kuhusu hali ya mtoto huyo, leo inatimia miaka mitatu tangu afariki Whitney Houston ambaye alikutwa pia ameanguka bafuni.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro
11 Feb 2015

Post a Comment

 
Top