Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Hizi ndivyo lori hilo lilivyoharibika


WATU watatu waliokuwa wamepakizana mishikaki wamekufa kwa kuteketea kwa moto mjini Iringa usiku wa kuamkia leo baada ya usafiri aina ya pikipiki (Boda boda)waliyokuwa wakisafiri kutoka mjini Iringa kuelekea Nduli nje kidogo na mji wa Iringa kugongana na lori aina ya fusu na kupelekea pikipiki hiyo kuwaka moto.

Wananchi wakishuhudia ajali hiyo ya Lori na boda boda 


Hii ndio pikipiki iliyoteketea kwa moto baada ya ajali 

Ajali hiyo imetokea majira ya saa 2 usiku wa jana  wakati boda boda hiyo ikiwa katika mwendo mkali kugongana na lori hilo ambalo pia lilikuwa katika mwendo na kusababisha vifo hivyo . 

Mashuhuda wamesema kuwa kijana mmoja ambae inasadikika ndie dereva wa boda boda hiyo ametambuliwa kwa jina moja la Julius huku wengine wawili bado kutambuliwa . 
Kutokana na ajali hiyo mbali lori hilo upande wa mbele ngao yake ilipinda huku eneo hilo la mbele likiharibika vibaya mfano wa kugongana gari kwa gari na baada ya hapo pikipiki hiyo ilishika moto na kuteketea yote pamoja na watu hao ambao miili yao ilizimwa kwa mchanga na wasamaria wema.
Miili ya marehemu hayo imehifadhiwa katika chumba cha maiti cha Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa kwa utambuzi zaidi.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro
01 Feb 2015

Post a Comment

 
Top