March 17, 2025 09:44:59 PM Menu
 

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Mkazi wa Tabata Mawenzi, Remi Joseph (36) anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kumuua mkewe kwa kumkata kichwa kwenye nyumba ya wageni ya Friends Corner ya jijini Dar es Salaam.
Aliyeuawa ni Josephena Moshi (35), ambaye alikatwa kichwa na kuchomwa na kitu chenye ncha kali kifuani wakiwa kwenye nyumba ya wageni ya Friends Corner.
Akihojiwa kuhusiana na tukio hilo, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa  Kinondoni, Augustine Senga, alikiri kutokea mauaji hayo.
Senga alisema mwanamke huyo alifariki papo hapo baada ya kushambuliwa na kwamba chanzo cha mauaji hayo hakijafahamika na uchunguzi unaendelea.
Kamanda alipoulizwa kuhusiana na mtuhumiwa huyo kutaka kujiua, alisema kuwa uchunguzi unaendelea.
Bado ni mapema sana kueleza kila kitu hayo niliyokueleza ni taarifa za awali kwani na huyu mtuhumiwa amekutwa na majeraha shingoni, hivyo masuala ya kazi yake na sababu vinachunguzwa:- Senga.
~NIPASHE

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro
01 Feb 2015

Post a Comment

 
Top