Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Mwigizaji na mwogozaji wa filamu za hapa bongo, Jacob Stephen ‘JB’ amefunguka ya moyoni  juu ya upendo wake kwa mke wake na kuendelea kudumisha ndoa yao.

JB tofauti na mastaa wengi wa hapa bongo, amemuweka na kumwambia waziwazi mke wake wa ndoa maneno  ya upendo ambayo huwafanya mashabiki wake wote kkujua na kumtambua shemeji yao au wifi yao.

JB leo hii ameweka picha hiyo mtandaoni akiwa na mke wake na kuandika maneno haya;

“Mke wangu,rafiki yangu, nampenda sanaa. Siku kama ya leo tuliingia kanisani tukatoa kiapo cha maisha,hakuna kilicho badilika wala kitakacho badilika mpaka kifo kitakapo tutenganisha. NAKUPENDA SANA MKEWANGU,Mungu azidi kuibariki ndoa yetu”. JB alimaliza.

Tunakupongeza JB kwakuendelea kuheshimu na kuitunza ndoa yako, tunawatakia baraka katika maisha yenu.
~Bongomovies

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top