Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Jeshi la polisi wilayani Kahama Mkoani Shinyanga linawasaka wanawake watatu kwa tuhuma za kuwalisha chips yenye madawa ya kulevya, madereva wawili wa roli la mafuta kutoka Dar es Salaam kwenda nchini Rwanda.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha amesema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia mwaka mpya katika maeneo ya Phantom mjini Kahama, baada ya madereva hao kuokolewa asubuhi na wasamaria wema.

Kamugisha amesema madereva hao waliwapatia Lifti wanawake watatu waliodai wanatoka Misigri Mkoani Singida kwenda Nyakanazi Mkoani Kagera lakini walipofika wilayani Kahama walishuka kwenda kununua chips.

Katika tukio hilo wanawake hao baada ya kununua chips walirudii kwenye gari wakawapa madereva hao ikiwa imefungwa kwenye mifuko, baada ya kuila walilewa wote na wanawake hao walianza kutaka kunyonya mafuta kutoka kwenye tenki la roli hilo.

Hata hivyo Kamugisha amesema juhudi hizo za kuiba mafuta hayo ziligonga mwamba baada ya kushindwa kufungua mfuniko wa siri ulikuwa kwenye tenki la mafuta hayo mpaka ilipofika asubuhi wanawake hao walitelekeza roli hilo na kutoroka pasipo julikana.

Aidha Kamanda kamugisha amewataja madereva hao kuwa na Birari Muhamed (49) mkazi wa mbezi Dar es salaam pamoja na msaidizi wake Amiri Salum (20) ambaye pia ni mkazi wa Dar es salaam, waliokuwa wakiendesha roli la mafuta namba T860 DCY aina ya IVECO na hali zao zinaendelea vizuri baada ya kupata matibabu katika hospitali ya mji wa Kahama.
Chanzo Kijukuu cha Bibi Blog

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top