March 19, 2025 10:52:04 AM Menu
 

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Nyota wa Barcelona kutoka kushoto, Luis Suarez, Neymar na Lionel Messi wakishangilia baada ya wote kufunga mabao katika ushindi wa 3-1 dhidi ya Atletico Madrid
BARCELONA imeibuka na ushindi mnono wa mabao 3-1 katika La Liga dhidi ya Atletico Madrid usiku wa kuamkia leo Uwanja wa Camp Nou.

Shukrani kwao, wafungaji wa mabao hayo, Mbrazil, Neymar, dakika ya 12, nyota wa Uruguay, Luis Suarez dakika ya 59 na Muargentina Lionel Messi dakika ya 87. Bao pekee la Atletico limefungwa na Mario Mandzukic dakika ya 57 kwa penalti. Katika mchezo huo, Neymar aliumia kifundo cha mguu kiasi cha kutokwa damu baada ya kugongana
na beki wa kati wa Atletico, Jose Gimenez.

Neymar alitolewa nje kwa machela na kutibiwa kwa dakika kadhaa kabla ya kurejea uwanjani.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro
12 Jan 2015

Post a Comment

 
Top