Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Video nyingi zilizoongozwa na kutayarishwa na Nisher zimefanyia usiku na ana sababu maalum ya kufanya hivyo. 

Kwa mujibu wa muongozaji huyo wa Arusha, video za usiku zinampa nafasi ya kuutumia ujuzi wake ipasavyo kwakuwa si rahisi kuzifanya.

Kwangu mimi naona kushoot mchana ni rahisi sana, yani sihitaji kuumiza kichwa, sababu mwanga wa jua unatoka sehemu moja so issue ni kubadilisha tu position ya character wangu, na kubalance mwanga kwenye camera yangu. Na mara nyingi nashoot flat ili niweze kupata details zaidi wakati wa grading,” anafafanua Nisher.

Pili sihitaji vitu kama taa au jenereta, au crew kubwa sana ya taa sababu mwanga wa jua ni mkubwa sana so ntatumia tu reflectors, unless na shoot kwenye vivuli. 3.Kushoot usiku ni kazi zaidi kwa upande wangu kwasababu hapo ndo ile taaluma ya CINEMATOGRAPHY inapotakiwa zaidi, unatakiwa kuumiza kichwa zaidi. Unahitaji kujua unatumia taa za aina gani, camera ya aina gani je unaweza kushoot nayo usiku usipate noise? Unahitaji lens za aina gani, kunaweza kutokea tatizo la flickering sababu ya light frequency unadeal nalo vipi, so inanifanya niwe CREATIVE na AWARE zaidi kujua nahitaji picha ya namna gani (LOOK),” ameongeza Nisher.

Huwa napenda kufuatilia video za nchini Marekari zaidi wanavyo fanya. Unakuta mtu ana tumia masaa kuandaa Lights ili kuweza kupata Lighting sahihi. Mimi naona kutumia taa ni kama moja wapo ya sanaa, na ni ngumu sana, ndo maana naipendelea zaidi. Ndo maana unakuta Wabongo wengi wamezoea video za mchana sababu directors wabongo hawapendi kuumiza kichwa kwenye Lighting na Cinematography sababu ni kazi ngumu kuliko zote kwenye video production, inakula time na inahitaji skill ya hali ya juu. Muulize Professional yeyote atakwambia!! Unachokiona kwenye video zangu sio giza, ni aina picha inayotakiwa kwa video husika. Kila moja ina style yake, kutokana na lighting inayofanyika.”

Unazungumziaje sababu za Nisher?

~Bongo5
Ungana nasi katika  Facebook na Umechekeshwa

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro
13 Dec 2014

Post a Comment

 
Top