April 4, 2025 07:58:12 PM Menu
 

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Muigizaji wa filamu hapa nchini, Elizabeth Michael “Lulu” amefunguka kwa kuandika mtandaoni kuwa atabadilisha jina lake na kuitwa Luppy iwapo Happiness Watimanywa ambae ni Miss Tanzania mwaka 2013 anaeshiriki shindano la Miss World 2014 ataibuka mshindi wa taji hilo.

Hili amelisema mapema kabisa ili yasijemkamkuta kama yaliyomkuta baada ya kusemekana kuwa alitaka kujiweka kwa mshindi wa BBA 2014, Idris baada ya kuibuka mshindi.Pia Lulu alisisitiza watu waendelee kumpigia kura Happines ambae kwasasa ameingia kwenye kumi bora upande wa Miss World People’s choice.

Ikiwa zimebaki saa takribani 26 tu zoezi la upigwaji kura za miss world kufungwa. Tumpigie kura za mwisho mwisho mrembo wa taifa letu ambae ameipeperusha bendera yetu vizuri na kutokana na kura zetu ameingia top 10. Nchi 3 za afrika zimeingia top 10 ambazo ni Chad na South Africa na Tanzania. Ushindani hapa ni mkubwa sana. Let us vote for her.

Jinsi ya kumpigia kura Mrembo wetu Happines ni Hivi:
1)kutoka AppStore au PlayStore Download app ya MISS WORLD
2)Kisha chagua Your Top3....Browse Contestants, mchague Happiness Watimanywa kutoka Tanzania na wengine wawili,kisha
3)bonyeza VOTE NOW
“Mtanzania mwenzangu Kura Yako Ndo ushindi wa Happy Na Ushindi wa Happy ndo Kick Ya jina Langu Jipya...!” Lulu alimaliza.
Ungana nasi hapa Facebook na Umechekeshwa

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro
13 Dec 2014

Post a Comment

 
Top