Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
art-radio-generic-620x349

Hekaheka ya leo December 16 inatoka Dar es Salaam ambapo msichana mmoja alijifungua mtoto chumbani kwake ndani ya nyumba aliyopanga na kwenda kumtupa mtoto ndani ya shimo la choo huku akieleza kuwa sababu iliyomfanya aamue hivyo ni kitendo cha mwanaume aliyempa ujauzito huo kumtelekeza.

Mtoto wa mwenye nyumba ambapo msichana huyo anaishi aligundua kutupwa kwa mtoto huyo baada ya kuingia kujisaidia katika choo hicho na kusikia sauti ya mtoto akilia kutoka ndani ya shimo la choo hicho, akamwambia mama yake ambaye alitoa taarifa kwa mume wake pamoja na mjumbe ambaye alitoa taarifa kituo cha Polisi.
Baada ya Mjumbe kufika na Polisi alikuta tayari majirani walikuwa wameanza jitihada za kuchimba shimo ili kumtoa mtoto huyo, baada ya kufanikiwa kumtoa akiwa mzima walimpeleka Hospitali ya Mwananyamala.
Mtoto huyo ni mzima, baada ya msichana huyo kufikishwa Hospitalini hapo alipewa mtoto wake na kuanza kumnyonyesha.
Unaweza kuisikiliza Hekaheka hiyo hapa.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top