Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Mastaa wa Tanzania Nasibu Abdul a.k.a Diamond Platnumz na Omary Nyembo a.k.a Ommy Dimpoz, nyimbo zao zimetajwa kuwania tuzo za HiPipo Music Awards (HMA2015) za Uganda zinazotarajiwa kutolewa mwakani.
Ommydiamond
‘Number One’ (original) ya Diamond na ‘Ndagushima’ ya Dimpoz zinachuana na nyimbo zingine za Afrika Mashariki kwenye kipengele kimoja cha East Africa Super Hit.
Nyimbo za Ommy na Diamond zitakuwa zikichuana na ‘Nishike’ ya Sauti Sol na ‘Kioo’ ya Jaguar. Nyimbo nyinginne kwenye kipengele hicho ni Baramushaka – Knowless, Sitya Loss – Eddy Kenzo, Tayali – Urban Boys Ft Iyanya pamoja na Love You Everyday – Bebe Cool.
Tuzo za HiPipo Music Awards 2015 (HMA2015) zitatolewa siku ya Jumamosi Feb.7, 2015
Chanzo: HiPipo

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro
12 Dec 2014

Post a Comment

 
Top