Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Waokoaji na wakazi wakikutana katika eneo la tukio la mlipuko wa bomu katika soko katikati ya mji wa Jos
Watu wasiopungua 30 wameuawa katika milipuko miwili ya mabomu iliyotokea karibu na kituo cha basi katika mji wa Jos, ulioko katikati mwa Nigeria. 

Walioshuhudia wanasema, bomu la kwanza lilitegwa kwenye kibanda cha kuuzia chakula na la pili karibu na mlango wa kuingilia katika soko la Termus kwenye mji huo.
Duru za usalama za Nigeria bado hazijasema milipuko hiyo ya mabomu imesababishwa na kundi gani, lakini kundi la Boko Haram ndilo limekuwa likishambulia na kutega mabomu katika maeneo mbalimbali ya Nigeria.
Mwezi Mei mwaka huu, kundi hilo la kigaidi lilitega milipuko iliyopelekea kufariki dunia watu 118 kwenye mji huo wa Jos.
 Watu zaidi ya 10,000 wamepoteza maisha kutokana na mashambulizi na milipuko iliyofanywa na kundi la kitakfiri la Boko Haram nchini Nigeria tangu mwaka 2009.
Source BBC

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top