March 18, 2025 07:05:19 AM Menu
 

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Tugawane Maumivu ni filamu mpya iliyotoka hivi karibuni kutoka kwa muigizaji na muongozaji wa filamu, Nice Mohammed  maarufu kama Mtunisy. 

 Akizungumzia maendeleo ya kazi hii sokoni, Mtunisy aliwashukuru mashabiki na wapenzi wote aliomuunga mkono kwa kununua kazi yake na kuwaomba waendelee kumuunga mkono.

 “Ahasanteni wapendwa kwa sapoti yenu kubwa mlioionyesha kwa kununua film yangu mpya hakika nimeamini huwezi kuchukiwa na wote hii imedhihilisha ktk kz yangu hii ya TUGAWANE MAUMIVU na kuifanya iwe ndio habari ya mjini kwa sasa nawaomba endeleeni kuniunga mkono wapendwa mungu awabariki sana amen ijumaa kareem”.
Mashabiki wengi waneonysha kuipenda na kuikubali kuwa ni  kazi nzuri na ina dhana mpya ambayo imewagusa wengi, akizungumzia mrejesho huu Mtunisy alisema “Nashukuru ndugu zangu siku hizi mtu akikuumiza nawe muumize tu mradi mugawane maumivu iweje yeye akuumize na asiumie bwana!tuumizane tu habari ndio hiyo”.

Hiyo ndio dhana nzima ya filamu hiyo ya Munisy, TUGAWANE MAUMIVU ambayo imejumuisha wakali kama, Chuchu Hans, Rammy Galis, Mukly Ismail na Nice Mohammed mwenyewe. imefanyika chini ya STEPS entertainment.

Jipatie nakala yako halisi kumsapoti wasanii wetu wa Tanzania.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro
12 Dec 2014

Post a Comment

 
Top