Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


MWANAMUZIKI wa muziki wa Bongo Fleva nchini, Nasib Abdul, Diamond Platinum anashindana na aliekuwa mpenzi wake Wema Sepetu katika kuwania Tuzo ya Mtu mwenye ushawishi mkubwa katika mitindo. 
Tuzo hiyo zitatolewa kwenye Onesho la Mavazi la Swahili Fashion 2014 linaloandaliwa na Kampuni ya 361 Degrees na zitatolewa siku ya mwisho katika onesho la Swahili Fashion Week litakaloanza Desemba 5 hadi 7 mwaka huu.
Katika shindano hilo wanaoshindana wengine ni pamoja na Mwamvita Makamba            ambae namba yake ya kupigiwa kura ni SFW SY 01, Diamond Platnumz       SFW SY 02, Millen Magesse   SFW SY 03, Mohamed Dewji  SFW SY 04 na Wema Sepetu           SFW SY 05.
Pia Diamond anashindana katika kipengele cha wanaume wenye kuongoza huku namba yake ya ushiriki ikiwa ni SFW SMP 01 na anaochuana nao katika kipengele hicho ni pamoja na Luca Neghest        SFW SMP 01,  Baraka Shelukindo       SFW SMP 03, Noel Ndale        SFW SMP, Rio Paul      SFW SMP 05 na           Juma Juxx        SFW SMP 06
Akizungumza na waandishi wa habari mratibu wa tuzo hizo, Haruna Ibrahim alisema kuwa kwa mwaka huu kuna ushindani mkubwa katika kila kipengele. Aliongeza kuwa Meneja wa Msanii Wema Sepetu, Martin Kadinda nae anawania kipengele cha Mbunifu bora wa mchango katika tasnia hiyo ambapo anashindana na  akina PSJ Couture    SFW MWD 01.


Martin Kadinda.          SFW MWD 02 Mtani Nyamakababi    SFW MWD 03, Manju Msitta  SFW MD 04 na Gabriel Mollel  SFW MWD 05.

Aliongeza kuwa pia kwenye kipengele cha mbunifu wa mavazi bora wa mwaka wanaoshindania Kadinda anashindana akiwa anaumana na akina Gabriel Mollel        SFW ID 02, An Nisa Abayas    SFW ID 03, Eve Collections            SFW ID 04

Alisema kuwa kwa upande wa Baileys, mwanamitindo bora wa kike kwa mwaka huu wanaoshindana ni            Jamilla Nyangassa      ambae namba yake ya kupigiwa kura ni SFW FM 01, Gyver Meena            SFW FM 02,  Jihan Dimachk      SFW FM 03, Neema Kilango  SFW FM 04,     Joceline Maro, SFW FM 05, Lethina Christopher            SFW FM 06.

Kwa upande wa wanamitindo bora wa kiume wanaoshindania tuzo hizo ni pamoja na Danny  David        SFW MM 01, Victor Casmir SFW MM 02,          Dietrich luhanga        SFW MM 03,  Ally Daxx          SFW MM 04.
Haruna aliongeza kuwa kwa upande wa Tuzo za Mwanamitido bora wa mwaka kwa Afrika Mashariki wanaoshindaniwa ni pamoja na Vivian Mutesi (UGANDA)    SFW EAM, Sharon Mirembe Sanya (UGANDA)          SFW EAM 02, Christina Masese (KENYA)   SFW EAM 03, Ajuma Nasenyana (KENYA)      SFW EAM 04                                                                                     

 Aliongeza kuwa kwa upande wa Tuzo ya Mbunifu wa mwaka wanaoshindania ni pamoja na Kiki's Fashion    SFW DY 01, Jamilla Vera Swai            SFW DY 02, Ailinda Sawe        SFW DY 03,An Nisa Abayas SFW DY 04, Manju Msita        SFW DY 05, Lucky Creations   SFW DY 06
Pia aliongeza kuwa kutakuwa na tuzo ya mwaka kwa mtaalamu wa urembo na nywele na wanaoshindaniwa ni pamoja na Rehema Samo      SFW HMA 01, Asila Makeup   SFW HMA 02, Glambox          SFW HMA 03, Lavie Makeup Studio            SFW HMA 04.

Pia wanaoshiriki katika kipengele cha kushindani tuzo ya vidani ni The Mabinti Center     SFW AD 01, Enjipai Jewelleries      SFW  AD 02, Florinyah Designs           SFW AD 03, Sairiamu  SFW AD 04, Linda August        SFW AD 05 na Nyumbani Designs SFW AD 06.

Watakaoshindania tuzo katika kipengele cha mbunifu wa Afrika Mashariki wanaoshindania ni pamoja na             Martha Jabo (Uganda)            SFW EAD 0, Afrostreet Kollektions (Kenya)    SFW EAD 02, Arapapa by Santa Anzo (Uganda)           SFW EAD 03, Akinyi Odongo (Kenya)  SFW EAD, Kiko Romeo (Kenya)           SFW EAD 05 na Mille Colliness (Rwanda)        SFW EAD 06.

Swahili Fashion Week na Tuzo za mwaka 2014 zinaandaliwa na 361 Degrees kwa usaidizi wa Hotel Sea Cliff, Sea Cliff Court, chini ya udhamini wa EATV, East Africa Radio, Baileys, Mercedes-Benz,  2M Media, Tanzania Printers LTD and Syscorp Media na Basata.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top