Ndoa tamu! Mkongwe wa sinema za Kibongo, Amri
Athuman ‘Mzee Majuto’ amesema kuwa, wasanii wa kike wamekuwa wakimpa
usumbufu kiasi cha kuifanya ndoa yake itetereke kutokana na kuvutiwa
naye kimapenzi.
Pasipo kuwataja majina, Mzee Majuto alisema mastaa hao wamekuwa
wakimsumbua kiasi cha kusababisha kero kubwa kwa mkewe na kumfanya
apoteze imani kwenye ndoa yake.
“Usumbufu upo wala siwezi kuwalaumu sababu mimi japo ni mzee lakini
ni mwanaume mzuri ambaye ninawavutia kutokana na mambo yangu
ninayoyafanya, kimsingi wanachotakiwa kuheshimu ni ndoa yangu,” alisema
Mzee Majuto.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro








Post a Comment
Post a Comment