LEGENDARY kwenye anga la sanaa Bongo, Vincent Kigosi
‘Ray’ kwa mara ya kwanza amefunguka kuwa mpenzi wake wa sasa, Chuchu
Hans ndiye kila kitu na kilichobaki ni ndoa tu.
Akizungumza na paparazi wetu, Ray alisema licha ya kupitia katika
changamoto nyingi za mapenzi lakini kwa Chuchu amefika na haoni tabu
kujinadi kwa mtu yeyote juu ya penzi lake hilo.
“Chuchu ndiye kila kitu kwangu, tunaendana kwa kila kitu hivyo
nitakaowaudhi kwa kumpenda yeye, wanisamehe,” alisema Ray.Ray kabla ya
kuwa na Chuchu, kwa nyakati tofauti alikuwa akitajwa kushea penzi la
mwigizaji Ruth Suka ‘Mainda’ na Blandina Chagula ‘Johari’.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment