Wiki
chache baada ya WhatsApp kutambulisha mfumo mpya ambapo iwapo unamtumia
message mtu inakuonyesha alama ya tick mbili za kijani na pia
inaonyesha muda ambao mtu uliyemtumia message hiyo ameisoma, tayari kuna
ndoa ambayo imeingia matatizoni kutokana na hilo.
Mwanaume mmoja Saudi Arabia ametoa
talaka kwa mkewe kutokana na kitendo cha mwanamke huyo kutokujibu
message aliyomtumia WhatsApp.
Mwanaume huyo amesema kitendo
kilichomkasirisha zaidi ni pale aliporudi nyumbani na kumkuta mke wake
akiwa busy anachat na marafiki zake kupitia mtandao huo wakati message
aliyomtumia yeye hakuijibu.
Jamaa huyo ameona kama kitendo hicho ni
dharau kubwa na hakuwa tayari kuendelea na ndoa hiyo ambayo imedumu kwa
miaka miwili tangu ifungwe.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment