Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
NDOA ni mpango wa Muumba ulio wazi kabisa kwamba,  wakati wa uumbaji wa Adam na Eva, ndiyo ndoa ya kwanza ilifungwa kwenye Bustani ya Eden.

Ndoa hiyo ilifungwa pale Mungu aliposema; ‘si vizuri kumwacha peke yake mtu huyu (Adam) tumfanyie msaidizi (Eva)’. Baada ya Mungu kumuumba Eva, akawaweka pamoja na kuwa mke na mume! MPANGO WA NDOA

Kwa hiyo kumbe, mpango wa ndoa kwa binadamu ni matakwa ya Mungu si ubunifu wa binadamu kama wengi wanavyofikiri.
Miaka ya hivi karibuni kumekuwa na msemo kwamba, kutokana na hali ngumu ya maisha ya ndoa, basi  wanaotaka kutoka (talaka) ni wengi kuliko wanaoingia au wanaotaka kuingia!
UTAFITI WA HARAKA
Watafiti wa harakaharaka wanadai kwamba, katika kila wanandoa kumi, saba wanataka ndoa zao zife ili wawe huru huku katika kila watu kumi wasio katika ndoa, watatu wanataka kuingia, saba hawataki!
UKWELI WENYEWE
Kama mtu atakuwa makini na kurejea kumbukumbu zake vyema atabaini kwamba, wanandoa wengi kutaka kutoka halafu wachache kuingia ni msemo uliojipatia jina kutoka kwa wale walioshindwa na ndoa zao na hivyo kupakaza uzushi huo ili ionekane ni kweli.
Ni kweli idadi ya ndoa zinazovunjika kwa mwaka ni nyingi lakini hazifikii idadi ya zinazofungwa kwa mwaka huohuo! Ndoa zinafungwa nyingi sana na wengi bado wapo ndani ya ndoa hata kama zinalegalega au zinakwenda mrama!
WANAOTAKA KURUDI
Utafiti wa hivi karibuni unaonesha kwamba, ‘watalaka’ kibao waliotoka ndoani miaka ya kuanzia 2005, sasa wanataka kurudi baada ya akili zao kuwaambia walibugi kutoka. Wapo wanandoa waliotoka baada ya kuamini kwamba wanakokwenda ndiko kwenye manufaa kuliko walipo lakini kumbe baada ya kufika huko walikoamini wakakuta hakuna kitu.
Wengine walitoka kwenye ndoa wakiamini wanakwenda kukuta magari, mali au fedha nyingi lakini baada ya muda waligundua magari yalikuwa ya kuazima, mali si za wahusika na pesa ni za msimu tu, hivyo kuona ni bora kurudi kuliko kuendelea kuwa huko.

KIKWAZO
Idadi ya hawa inaweza kuonekana ni ndogo kwa sababu wengi wanaotaka kurudi wanashindwa kwa vile wanakuta ‘nafasi imejaa’ na hivyo kuishi maisha ya usingo unaoambatana na majuto ni mjukuu.
Kama wanandoa wangepewa ‘riheso’ ya kuachana halafu siku moja wakakaa na kutafakari waendelee na kuachana au waghairi, kura ya wanaotaka kughairi zingekuwa chache sana na wanaotaka ndoa ziendelee zingekuwa za ushindi wa kishindo. 
NI FUNDISHO
Katika historia ya mwanadamu, kila afanyae uovu humkuta mabaya au hulipa uovu wake hapahapa duniani. Katika ndoa, mikasa mingi, hata kwenye sinema inaonekana kuwa, katika ndoa kila anayesababisha ikavunjika ndiye anayekutana na magumu mbele ya safari hivyo kukumbuka alikotoka! Ndiyo maana nasema wanaotaka kurudi ni wengi kuliko wanaotaka kutoka.
Ningependa hili likae mawazoni mwa watu kwamba, kumbe ndoa za siku hizi bado zinajikongoja kwa namna yake ndiyo maana wanaotaka kurudi ni wengi sana kuliko wanaotaka kutoka. Maisha ni magumu sana, ndoa ni za kuvumiliwa na kila mtu!!
MSISITIZO
Mara zote mimi nimekuwa nikisema kwamba, kama katika ndoa kila mmoja atachukua nafasi yake na kuikubali basi wanandoa watatimiza agizo la Mungu kwamba wawili waishi hadi kifo kiwatenganishe lakini mvurugano wowote hapo, kasoro zitaanza na ugumu wa moyo hutokea na hatimaye ndoa huvunjika.
Wengi wanaamini kuvunjika kwa ndoa kunatokana na wawili kutoelewana lakini ukweli ni kwamba kunatokana na mmoja wa wanandoa au wote wawili kutotambua nafasi yao.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top