Stori: Makongoro Oging’ na Haruni Sanchawa
SIKU chache baada ya Jeshi la Polisi Kitengo cha Kuzuia na Kupambana na Madawa ya Kulevya Tanzania kumkamata mfanyabiashara bilionea Mharami Mohamed Abdallah ‘Chonji’ mkazi wa Magomeni, Mtaa wa Kondoa jijini Dar akidaiwa kukutwa na unga, jeshi hilo linamhenyesha anayedaiwa kigogo mwingine wa unga ambaye ni mwanamke.
Christina Naphtali Kigaye mkazi wa Mikocheni anayehusishwa na biashara ya madawa ya kulevya.
Kamanda wa kitengo hicho, SACP Godfrey Nzowa, wiki iliyopita aliimbia Uwazi kwamba mwanamke huyo, Christina Naphtali Kigaye (pichani), mkazi wa Mikocheni, Dar alikuwa akitafutwa kwa muda mrefu na jeshi lake.
Kamanda Nzowa alisema, Christina amekuwa akitajwa na watu wengi wanaokamatwa na unga kuwa, yeye ndiye kigogo wa unga na amekuwa akiwabebesha mzigo na kuwatuma sokoni nje ya nchi.
Christina Naphtali Kigaye akiwa katika kituo cha polisi.
Kamanda Nzowa alisema siku ya tukio kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar, saa tatu asubuhi ya Oktoba 29, mwaka huu, mtuhumiwa huyo akitokea nje ya nchi alinaswa baada kitengo chake kutonywa na watuhumiwa wengine ambao tayari wameshakamatwa lakini wakawa wanaijua ratiba yake.
“Pamoja na kwamba anadai kuwa anafanya biashara ya kuuza nguo na simu lakini hizo amejiegesha tu. Kwa mujibu wa watuhumiwa waliokamatwa na unga wamemtaja kwa asilimia kubwa kujihusisha na biashara hiyo haramu.
“Kwa sasa upelelezi unaendelea dhidi yake na utakapokamilika hatua zaidi za kisheria zitachukuliwa ikiwa na pamoja na kumpandisha mahakamani,” alisema Kamanda Nzowa.
Habari zaidi kutoka ndani ya jeshi la polisi zinadai kuwa mwanamke huyo alipelekwa makao makuu ya kitengo cha kuzuia madawa hayo Kilwa Road na kuhojiwa maswali mengi ambayo yalimtoa jasho.
“Alihojiwa kwa saa nyingi hadi akatokwa na jasho, maswali yalikuwa mazito,” alisema mtoa taarifa wetu.
>>>>GPL
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Je Umezisoma Hizi?
- Tetemeko Lililotokea Jana Katika Mikoa Ya Kanda ya Ziwa Limeua Zaidi ya Watu 10 na Kujeruhi Wengine 12011 Sep 20160
Tetemeko la ukubwa wa mtikisiko wa kipimo cha Ritcher 5.7 limetokea katika mikoa mitatu nc...Read more ?
- Msafara wa Makamu wa Rais, Samia Suluhu wapata ajali Mtwara.09 Sep 20160
Msafara wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani, Mama Samia Suluhu Hassan ambao uliku...Read more ?
- Polisi Washuhudia Majambazi Yakitwangana Risasi.......Zakamatwa Shehena za Silaha na Vifaa vya Uhalifu06 Sep 20160
WATU watatu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wa kutumia silaha, ambao wamehusika kufanya matukio ...Read more ?
- Askari Magereza Atiwa Mbaroni Kwa Kuingia Wodini Akiwa Amelewa na Kisha Kuanza Kufyatua Risasi28 Aug 20160
POLISI mkoani Rukwa inamshikilia askari Magereza, Cleophas Chapaulinge kwa kosa la kulewa na k...Read more ?
- Polisi Mwingine Auawa Kwenye Mapambano Makali na Majambazi Huko Mkuranga27 Aug 20160
Ilikuwa ni kama filamu ya askari na maadui wakati askari wa Jeshi la Polisi walipopambana na wat...Read more ?
- RC Makonda: Polisi Mkikuta Mtu Yeyote Msituni Pigeni bila Huruma.......Haki za binadamu Wakiwauliza Waambieni waje Kwangu26 Aug 20160
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameliagiza Jeshi la Polisi kuwagonga na kuwapiga wah...Read more ?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment
Post a Comment