Stori: Gladness Mallya
Aibu kuu! Jamaa aliyejitambulisha kwa jina la Leonard Celestine ambaye anasomea upadri, anayemalizia masomo ya falsafa (philosophy) mwaka wa tatu katika Chuo cha Jordan mjini Morogoro, anadaiwa kuaibika gesti, kisa kikiwa ni mke wa mtu gesti.
Bw. Leonard Celestine aliyeaibika gesti na mke wa mtu.
TUJIUNGE GESTI
Kwa mujibu wa shuhuda wetu, tukio hilo la aina yake lilijiri hivi karibuni kwenye Gesti ya Silver Inn iliyopo maeneo ya Msamvu mjini Morogoro ambapo kijana huyo alipewa kipondo cha aina yake na kunyang’anywa kila kitu huku akiachwa kama alivyozaliwa na kulazimika kujisitiri na taulo la nyumba hiyo ya wageni.
KITU LAIVU!
Chanzo hicho kilidai kwamba, kijana huyo ambaye ni mwenyeji wa Iringa alikuwa na mchezo wa kutembea na huyo mke wa mtu tangu mwaka jana ambapo mumewe aliamua kumwekea mtego ulipofyatuka akanaswa laivu.
Bw. Leonard Celestine akijutia soo lililomkuta.
KUMBE!
Ilidaiwa kwamba, kama ilivyo seminari zote za Kikatoliki, mwanafunzi hutakiwa kukaa ndani lakini Leonard alidaiwa kuwa alikuwa akitoroka hasa siku za wikiendi au siku akiwa na vipindi vinavyoishia asubuhi na kwenda kukutana na mke huyo wa mtu na kujiachia naye kwani mumewe ni mtu wa kusafiri mikoani.
Ilisemekana kuwa kutokana na kujiachia huko mwenye mke aligundua na kuanza kumfuatilia tangu mwaka jana hadi alipowanasa hivi karibuni.
KIPIGO
Baada ya kunaswa, Leonard alipewa kipigo cha aina yake na watu ambao tayari walikuwa wameshaandaliwa na mwenye ‘mali’ ambapo alilia huku akiomba asamehewe ili yasije kuvuja akakosa upadri kwani ameshafika mbali.
Bw. Leonard Celestine akibanwa kwa maswali mara baada ya kupewa taulo kujisitiri.
APOKONYWA KILA KITU
Ilidaiwa kwamba, raia hao wenye hasira walimpokonya simu, begi lake lililokuwa na madaftari na nguo hivyo alitoka chumbani bila nguo na badala yake aliomba taulo kujisitiri.
PADRI ANASEMAJE?
Gazeti hili lilimtafuta Leonard kwa njia ya simu aliposomewa mashtaka yake alisema:
“Ni kweli hizo picha ni zangu, nalijua hilo tukio lakini ndugu mwandishi naomba usinitoe, nitakuwa nimekwisha kwani yule mwanamke hakuniambia kama ni mke wa mtu.”
Source GPL
Bonyeza hapa
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Je Umezisoma Hizi?
- Wanafunzi wa Shule ya Msingi Wajiuza kwa Shilingi 2000 Wateja Wao Wakubwa ni Madereva Bodaboda21 May 20150
UKISTAAJABU ya Musa utayaona ya Farao! Kumekuwa na madai ya baadhi ya wanafunzi wa shule ...Read more ?
- Pichaz: Pati 2 ya Padri wa Kanisa Katoliki Aliyenaswa Kichakani Akila Uroda na Kondoo Wake Jijini Dar19 May 20150
KISA cha Padri Anatoly Salawa (pichani) ambaye pia ana cheo cha Katibu Mtendaji wa Idara ya ...Read more ?
- Pichaz: Wasanii Chipukizi wa Bongo Wanaswa kwa Ufuska Live..!18 May 20150
SHABAASH! ‘Makinda’ wawili wanao penyapenya katika sanaa ya maigizo runingani wa Kundi la San...Read more ?
- Fumanizi la Aina Yake......Padri wa Kanisa Katoliki Anaswa Kichakani Akila Uroda na Kondoo Wake Jijini Dar15 May 20150
KAMA mti mbichi unatenda haya, itakuwaje kwa mti mkavu?! Ndivyo inavyoweza kutafsiriwa kwa K...Read more ?
- Mwanaume Afumaniwa Gesti Na Mke Wa Rafiki Yake14 May 20150
Kashikashi za kuambiwa umefumaniwa zisikie kwa mwenzako tu! Utakuta mtu mkubwa, bonge, lakini ak...Read more ?
- Sharobaro, Hausigeli Wanaswa Live Sebuleni kwa Boss.....So Latinga Polisi06 May 20150
Kijana mmoja mtanashati, aliyefahamika kwa jina la Faraja Adam mkazi wa Makongo jijini Dar ...Read more ?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
















Post a Comment
Post a Comment