Ubakaji! Msanii wa muziki wa Kizazi Kipya kutoka Kundi la Fagio la Chuma ambaye pia aliwahi kuitumikia B-Band chini ya Banana Zorro, Hafsa Ally, amesulubiwa kisha kunusurika kubakwa na baunsa aliyemtaja kwa jina moja la Mahamoud.
Msanii wa muziki wa Kizazi Kipya kutoka Kundi la Fagio la Chuma, Hafsa Ally akielezea mkasa uliomsibu kwa waandishi wa Global.
Akizungumza na gazeti hili wikiendi iliyopita, Hafsa alisema tukio hilo lilijiri hivi karibuni, mishale ya saa 8:00 usiku alipokuwa akitokea Ukumbi wa Delux uliopo Sinza-Kijiweni, Dar akielekea nyumbani kwake maeneo ya Kijitonyama.
Hafsa alisema, akiwa kwenye Bajaj, ndipo akashtukia kuna bodaboda inawafukizia kwa nyuma.
“Nilipoangalia nyuma nikaiona pikipiki ambayo nilihisi kama inatufukuzia, lakini kabla sijakaa sawa nikashangaa kumuona Mahamoud ambaye namfahamu kama baunsa na dereva wa bodaboda.
“Nilishangaa alipotufikia akiwa na mwenzake kwenye bodaboda alianza kunivuta nje huku Bajaj ikiwa kasi nikapata maumivu kwenye mbavu, michubuko mwilini na kunitegua bega,” alisema Hafsa na kuongeza:
“Baada ya kufanikiwa kuninyang’anya mkoba wangu alitaka kunibaka lakini nilipiga kelele kwa kushirikiana na dereva wa Bajaj niliyopanda ambapo wasamaria wema walijitokeza kunisaidia.
“Alipoona wananchi wamemzingira alitafuta upenyo na kukimbia ndipo nikaenda Kituo cha Polisi cha Urafiki (Dar) ambapo nilipewa fomu namba 3 (PF-3) kwa ajili ya kwenda kutibiwa.
“Nilikwenda kupata matibabu Hospitali ya Palestina (Sinza).
Hafsa Ally akionesha jeraha alilopata ubavuni wakati wa tukio.
“Baada ya kupatiwa matibabu nilimfungulia kesi yenye jalada namba URP/RB/8318/2014- JARIBIO LA UBAKAJI na tayari ametiwa mbaroni,” alisema Hafsa.
Bonyeza hapa
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Je Umezisoma Hizi?
- Mfungo Wamuepusha Amanda na Skendo...'Mwezi Huu Nguo Fupi za Kuwatega Wanaume Nimeziweka Pembeni'01 Jul 20150
Staa wa bongo movies, Tamrina Posh ‘Amanda’ amesema kuwa mfungo wa mwezi wa ramadhan...Read more ?
- Jingine Laibuka Kuhusu Rais wa FIFA..Kumbe Pia Alikuwa Anakula Demu wa Mchezaji Cristiano Ronaldo06 Jun 20150
Hali bado sio shwari kwa upande wa Rais wa FIFA, Sepp Blatter… Zimepita siku chache tu tangu atan...Read more ?
- Wellu Sengo Adaiwa Kutoka na Mume wa Mtu Mwigizaji Mwenzake Steven Nyerere02 May 20150
Mrekebishatabia wa Insta ameibua Mazito Kama ifuatavyoSaaaasa????? @stevenyerere2 ndo umeoa mke ...Read more ?
- Aunt Ezekiel Atoboa Kuhusu Wasanii wa Bongo Movies Kujitengenezea ‘Skendo’22 Apr 20150
Staa mrembo wa Bongo Movies, Aunt Ezekiel ‘Mama Kijacho’ amesema baadhi ya wasanii wa bongo movie...Read more ?
- Kipa wa Simba JR MANYIKA 'Anae Sema Naima Ananiua Kiwango Aje Acheze yeye Mimi Sio Khanisi Nina Haki ya Kuwa na Mpenzi'21 Apr 20150
BAADA ya Simba kufungwa mabao 2-0 dhidi ya Mbeya City katika mechi ya ligi kuu soka Tanzania bar...Read more ?
- Mume wa Mtu Apiga Picha za Utupu na Mchepuko..Picha Zasambaa Mtandaoni07 Mar 20150
KALOLI Dawa ambaye ni mume wa mtu, amedaiwa kujipiga picha za utupu akiwa na mchepuko wake uliofa...Read more ?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment
Post a Comment