Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Muigizaji maarufu wa filamu nchini Happy Nyatawe ambaye pia ni mfanyabiashara amewaasa wanawake wenzake kuacha kuwa magolikipa kwa wanaume na pia kuacha umbeya na badala yake wajikite katika kazi ili kujiletea maendeleo.

Akizungumza na Mpekuaji, Happy  amesema:
"Nashangaa wanawake ambao mpaka karne hii wanategemea wanaume Kwanini siku moja na wewe mpenzi wako au mumeo asifurahie msaada toka kwako ?
"Wanawake tunaweza kataa u-golikipa na vikao vya umbeya mitaani, u-busy unaepusha mambo mengi sana .Tuwe  bize  kusaka  pesa  na  si  kusuta  watu.

"Mimi mbali na biashara yangu muda mwingi napenda kupumzika nyumbani na kuangalia movie, yaani kazi za wenzangu  na  endapo itatokea msiba au sherehe hujumuika na wenzangu lakini naogopa sana kusutwa ndo maana sipend vigenge"
Bonyeza Hapa

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top