
Rais Museveni aliidhinisha sheria ya adhabu kali kwa Mashoga nchini Uganda mwezi Februari
Raia wa Uganda kutoka dini mbali
mbali hii leo wamekusanyika katika uwanja wa Kololo mjini Kampala kwa
maombi maalum na kutoa shukurani kwa Rais Yoweri Museveni kwa kutia
saini mswaada wa sheria unaozuia mapenzi ya jinsia moja.
Viongozi wa dini mbalimbali wakristo na waislamu wamehimiza waumini wao kujitokeza kwa wingi katika ibaada hiyo maalum.
Hii ni mara ya kwanza viongozi wa
dini mbali mbali nchini Uganda kujitokeza kwa pamoja na kuandaa Ibaada
maalum ya kumshukuru Rais Museveni na kuliombea taifa kuepuka vitendo
vya ushoga.
Rais Museveni aliidhinisha sheria hiyo ambayo raia wengi wa Uganda wameipigia debe sana.
Ibaada hiyo maalum inafanyika uwanja wa uhuru wa
Kololo mjini Kampala, baada ya karibu mwezi mmoja na nusu tangu rais
Yoweri Museveni kuiidhinisha
Tangu Rais Museveni kuidhinisha sheria hiyo
kumekuwa na shinikizo kubwa kutoka kwa mataifa ya Magharibi yakimtaka
kubadili msimo wake, huku baadhi ya mataifa yakipunguza msaada kwa
Uganda.
Lakini raia wengi wa Uganda walimsifu Rais Museveni kwa hatua yake.
Chanzo bbcswahili. Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro







Post a Comment
Post a Comment