Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Wahamiaji wengi wamekufa maji wakitokea LIbya
Wahamiaji wengi kutoka Libya wameripotiwa kupoteza maisha yao baada ya mashua waliyokuwa wakisafiria kuzama ikielekea upande wa Italia.
Kwa mujibu wa wanajeshi wa majini wa Libya, watu hao walikuwa wakijaribu kuvuka kuelekea Ulaya.

Msemaji wa majeshi ya majini ya Libya, Ayub Qassem amethibitisha watu 36 wameokolewa baada ya mashua yao iliyokuwa imebeba watu 250 ilipozama karibu na eneo la Tajoura, mashariki mwa Tripoli.
Asilimia kubwa ya wahasiriwa ni wanawake na watoto
Hata hivyo, amefichua ya kwamba maiti nyingi bado zinaelea baharini.
Mkasa huu umetokea wiki chache tu baada ya mashua nyingine tatu kuzama mfululizo katika njia ya baharini inayotoka Libya hadi Italia.
Kumekuwa na ongezeko la watu wanaoikimbia nchi ya Libya mwaka huu kutoka na ghasia zinazoshuhudiwa, huku walunguzi wa binadamu wakipata fursa ya kutekeleza uhalifu wao.
Waasi wamekuwa wakipigania udhibiti wa miji na vituo muhimu nchini Libya.
Makundi hasimu ya waasi wamekuwa wakipigana wakijaribu kutawala sehemu kubwa ya taifa hilo
Wanajeshi wa majini wa Libya wamelalamikia ukosefu wa vifaa na uwezo wa kutosha wa kukabiliana na mikasa.
Wamedai imewabidi kuazima mashua kutoka kwa wavuvi na kampuni nyingine.
Bw. Qassem amefafanua ya kwamba wengi wa wahamiaji hao walikuwa waafrika na pia jinsia ya kike.
Chanzo bbc
Bonyeza hapa like page yetu.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top